Site icon Bongo Plus

#JKT Tanzania yatinga rasmi Ligi Kuu 2023/24

Matokeo ya sare ya 1-1 ya Pamba dhidi ya Mbuni leo Aprili 22 imeihakikishia JKT Tanzania kupanda Ligi kuu licha ya kupoteza mchezo wake ugenini mbele ya Kitayosce kwa mabao 3-2.

JKT inarudi rasmi Ligi Kuu ikiwa na michezo mitatu mkononi ambapo pointi 62 ilizonazo zinairuhusu kuungana na miamba ya soka nchini, Yanga na Simba msimu ujao.

Vita imebaki kwa Kitayosce na Pamba kusaka mmoja wapo wa kuungana na Maafande hao kupanda moja kwa moja.

Exit mobile version