ASA NI ZAMU YA WANANCHI WA SONGWE, KAENI TAYARI WA SAUTI 3 ZA RADI
Baada ya kazi kubwa iliyofanyika Mkoani Rukwa na wananchi kukubali na kusadiki katika misingi ya Chama Cha Mapinduzi ambapo kwa kauli moja wametuthibitishia kutoyumbishwa na kuendelea kuunga mkono Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Sasa ni zamu ya wananchi wa Songwe ambapo sauti 3 za radi zikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC – Oganaizesheni Ndugu. Issa Haji Gavu , kwa umoja wao wataunguruma.

