Site icon Bongo Plus

Pole Pole nimekuwa na kikao na Rais wa Chama cha Wakalimani nchini Cuba (ACTI) Bi. Gretchen Gonzales ambaye tumezungumza pamoja na mambo mengine kuimarisha mahusiano ya kati ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Chama cha ACTI.

Tarehe 23 Juni 2024 ni nimekuwa na kikao na Rais wa Chama cha Wakalimani nchini Cuba (ACTI) Bi. Gretchen Gonzales ambaye tumezungumza pamoja na mambo mengine kuimarisha mahusiano ya kati ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Chama cha ACTI.

Kama sehemu ya kutambua mchango wa ACTI katika kukuza taaluma ya lugha na kama sehemu ya malengo ya msingi ya Ubalozi ya kukuza Utamaduni na Lugha, Ubalozi na ACTI wataendesha shindano la wanafunzi wa Chuo Kikuu wanaosomea lugha, uandishi wa habari na ukalimani, ambapo kwa mara ya kwanza kiswahili kitakuwa lugha mojawapo itakayotumika.

Ubalozi utakuwa mbia na mhisani wa mashindano haya na utatoa nafasi ya mafunzo kwa washindi wa lugha ya kiswahili kufanya kazi na Ubalozi katika mafunzo ya kiswahili yanayoendelea katika Chuo Kikuu cha Havana sambamba na zawadi mbali zikiwemo Kamusi za Kiswahili na Kihispaniola.

Huu ni muendelezo wa Ubalozi kuendelea kupeleka mbele agenda ya lugha ya kiswahili Kimataifa.

Exit mobile version