📌 Awahimiza wananchi wa Namonge kujitokeza kupiga kura Oktoba 29
📌 Asema shilingi bilioni 200 kukopeshwa kwa vijana
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Bukombe, Ndugu Doto Mashaka Biteko amewaasa wananchi wa Kata ya Namonge, kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais kwa kuwa ndiye mwenye nia thabiti ya kuwaletea maendeleo.
Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 9, 2025 katika mkutano wake wa kunadi sera kwa wananchi wa Kata ya Namonge wilayani Bukombe mkoani Geita.
Amesema awali sekta zote katika kata ya hiyo zilikuwa zikisuasua kimaendeleo ikilinganishwa na maendeleo yaliyofikiwa sasa
“Kata hii haikuwa na barabara ya kutoka Uyovu – Namonge – Nyalamandula haikuwa na zahanati wala shule za kutosha hivyo ilikuwa na maendeleo duni” amesema Dkt. Biteko.
Amesema jitihada zilizofanywa na Serikali ya Rais Samia katika kuwaletea maendeleo wananchi hao ni kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati na kituo cha afya.
“ Nataka niwahakikishie mkinichagua tutaongeza wodi na zahanati, tunataka watu wa Namonge waishi kama Watanzania wa daraja la juu, Tutahakisha tunaongeza shule, kuna vijiji havikuwa na shule na tumejenga shule mpya. Tumekuja hapa kuomba kura ili tumchague Rais Samia kwa vile ni kumchagua yeye ni kuchagua maendeleo,” amesema Dkt. Biteko.
Ameelezea matarajio ya CCM ni kuifanya Kata ya Namonge iwe kituo cha kilimo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara na hospitali.
Pia, amesema CCM ikipata ridhaa ya kuongoza katika miaka mitano ijayo Serikali itatoa shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kuwakopesha vijana ili wazitumie kwa kufanya biashara sambamba na kutoa mikopo kwa wanawake na watu wenyeulemavu.
“Namonge ina wapiga kura zaidi ya 30,000 hivyo nawaomba Oktoba 29 mwaka huu tujitokeze kwa wingi tukampigie kura Rais Samia. Tunachotaka ni maendeleo na nataka kuwahakikishia Rais Samia anatupenda mno Bukombe na mwezi Oktoba atakuja hapa. Heshima pekee tutakayompa Rais wetu ni kumpigia kura kwa wingi, msiniangushe,” amesisitiza Dkt. Biteko.
Akimnadi mgombea udiwani wa Namonge, Mlalu Bundala amesema ni mtu makini anayejua shida za wananchi na
