Basi litaondoka nchini kwenda Zambia tarehe 13, Septemba saa 1 usiku na tutafika Ndola, Zambia tarehe 15, Septemba. Tarehe 17, Septemba baada ya mechi basi litaanza safari kurudi Tanzania. Kwa yeyote ambaye anataka kuungana nasi afike ofisini. Kwa kila mtu gharama ni Tsh. 200,000 na anatakiwa kuwa na pasi ya kusafiria na kadi ya manjano. Mwisho wa kupokea nauli ni tarehe 10, Septemba.”- Ahmed Ally
Tumerejea mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo unaofata dhidi ya Power Dynamos. Wachezaji wote wamerejea isipokuwa golikipa Ayoub kutoka Morocco ambaye anarejea leo na moja kwa moja atajiunga na wenzake.”- Ahmed Ally. #WenyeNchi #NguvuMoja
Tuna siku nyingi za kufanya mazoezi na hivyo menejimenti inaangalia namna gani kikosi kitaweka kambi ya kujiandaa. Mazungumzo yamejikita katika sehemu mbili, moja kuweka kambi kwenye nchi za jirani au tuweke kambi ndani ya Tanzania katika maeneo mengine
“Taarifa njema ni kwamba Aubin Kramo na Henock Inonga wamepona na wamerejea mazoezini na wenzao.

