Site icon Bongo Plus

Aigiza Mshtuko wa Moyo Asilipe Bili.

: Jamaa mmoja nchini Hispania amekamatwa kwa kusingizia kupata mshtuko wa moyo kwenye mgahawa wa kifahari ili kuepuka
kulipa bili yake, Polisi wa Hispania wamesema Mtu huyo (50) jina limehifadhiwa, amekuwa akidanganya mara kwa mara katika migahawa ya
aina hiyo.

Safari hii amekatwa huko jijini Alicante baada ya kujaribu kuondoka kwenye
mgahawa mmoja bila kulipa huku akijifanya mgonjwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa insider, hilo lilikuwa ni tukio la 20 ndani ya mwaka mmoja, na hivyo kufanya ajulikane kwa polisi wa eneo hilo.

Katika tukio la hivi majuzi, mwanamume huyo aliagiza kinywaji na chakula huko El Buen Corner,
ambapo alitakiwa kulipa dola za Marekani $36.75 (takribani Sh93,000 jambo ambalo hakufanya.

Msimamizi wa mgahawa huo, Moisés Doménech, ameuambia mtandao wa EFE kwamba mfanyakazi mwenzake alimwona mtu huyo akijaribu kuondoka
bila kulipa na hivyo kumfahamisha kuhusu suala hilo.

Alipoulizwa juu ya malipo, mteja huyo alidai kuwa alikuwa anaenda chumbani kwake hotelini hapo, kuchukua pesa na kwamba angerudi kulipa, hata hivyo, wahudumu hao walimgomea kuondoka bila kulipa, meneja huyo amesema.

Inaelezwa kwamba baada ya kuona kazuiwa, alijidondosha kana kwamba amepata mshtuko wa moyo.

Hata hivyo wafanyakazi wa mgahawa huo hawakukubaliana na ujanja huo, hivyo waliwaita polisi, ambao mara baada ya kufika, walimtambua Msemaji wa Polisi wa Alicante amethibitisha
kwamba mtu huyo “Amewahi kukamatwa mara kadhaa jijini humo kutokana na matukio ya aina hiyo.

Exit mobile version