
Brianna LaPaglia, maarufu kama “Chickenfry” ameshangaza wengi kwa kudai kuwa aliyekuwa mpenzi wake, Zach Bryan, alimpa ofa ya dola milioni 12 kama angekubali kusaini makubaliano ya kutofichua siri (NDA) kuhusu uhusiano wao na sababu za kuachana.
Brianna LaPaglia alieleza hayo kwenye kipindi chake cha “BFFs” podcast.LaPaglia, mwenye umri wa miaka 25, alisema timu ya Bryan ilimpa ofa hiyo ili aache kuzungumzia mambo yoyote kuhusu uhusiano wao kwa umma. Ingawa alikiri kuwa ofa hiyo ilikuwa na pesa nyingi, LaPaglia alisema hakuwa tayari kuchukua “fedha chafu” ili kuficha mambo aliyopitia.
“Nina furaha pale nilipo, na sitaki kuchukua pesa hizo,” alisema. Pia, alisema kuwa ingawa familia yake walimsihi akubali kwa kuwa hawana fedha, alihisi kwamba kukubali kungeenda kinyume na maadili yake.
Mwisho wa kipindi, LaPaglia aliongeza kuwa timu ya Bryan ilimpa ofa ya nyumba ya kifahari jijini New York, lakini bado alikataa.
Unaweza Kukataa Ofa Kama Hii Hata Kama Ex Wako Alikufanyia Vibaya?

