Site icon Bongo Plus

Akutwa na Hatia Yakumuuwa Aliyegundua Kabadili Jinsia.

San Francisco, Marekani Leniyah Butler mfanyakazi wa ngono mwenye umri wa miaka 21 amepatikana na hatia ya mauaji ya  Hamza Walupupu kufuatia mzozo uliozuka baada ya tendo la ngono.

Tukio hilo lilitokea Novemba 2023 katika eneo la Crissy Field, karibu na Daraja la Golden Gate.

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, Walupupu alimchukua Butler kwa gari lake na baada ya kujadiliana kuhusu bei na huduma, walielekea Crissy Field. Butler alisema alihisi kutolewa katika mazingira yake ya kawaida baada ya safari ya dakika 20 kwenda eneo hilo.

Baada ya tendo la ngono, Butler alimweleza Walupupu kuwa yeye ni mtu wa jinsia iliyobadilishwa (transgender).

Walupupu alikasirika na kudai arejeshewe pesa, hali iliyosababisha mabishano makali. Katika hali ya kujitetea Butler alimpiga risasi usoni kwa bastola aliyokuwa nayo kwenye mkoba wake.

Kisha aliburuta mwili hadi eneo la maegesho, akaondoka na gari la Walupupu hadi Kiska Road, Hunters Point, na kumpigia mama yake simu akiomba msaada.

April 1, 2025, Butler alipatikana na hatia, na hukumu yake imepangwa kutolewa mwezi Juni 2025.

Exit mobile version