Je, una heshimu muda wa kupumzika na mpenzi wako? Mfano wa kuigwa hapa ni Alicia Keys ambaye alizikataa ($9 million) sawa na zaidi ya TSh. BILIONI 24 baada ya kupewa ofa hiyo ya kutumbuiza kwa dakika 9 tu.
Swizz Beatz amekaririwa akisema, kampuni hiyo ilimtafuta Alicia Keys na kumpa ofa hiyo nono lakini Keys aliipiga chini akidai kwamba, tarehe hiyo atakuwa bize akitumia muda wake vizuri na mumewe! 🤯
Swizz anaendela zaidi kutueleza kwamba, Keys angeweza kukataa hata ingekuwa ($100 million) kama tu dili hilo litaingilia muda wao binafsi, kwani vipaumbele vya maisha yao ni zaidi ya pesa