Kwa Mujibu Wa TMZ, Dereva aliyemgonga na kumuua Baba Wa Rapa Nicki Minaj miaka 5 iliyopita, amekubaliana Na Familia kumaliza kesi ya madai ya kifo hicho nje ya mahakama.
Katika kesi hiyo, Carol (Mama Wa Nicki Minaj) alikuwa akiomba fidia kwa kumpoteza mume Wake, Akidai hasara ya upendo, msaada Na Ushirikiano aliokuwa akiupata kutoka kwake.
Makubaliano haya yamefikiwa Mapema Mwezi March baada ya Dereva (Polevich) kujaribu kumuita Nicki Minaj mahakamani ili ahojiwe (deposition). Ambapo Alitaka kumuuliza kuhusu Mashairi ya nyimbo zake yanayohusu utoto wake, akijaribu kuonesha kwamba ndoa ya wazazi wake haikuwa nzuri sana, jambo ambalo aliamini lingepunguza kiwango cha fidia anachopaswa kulipa.
Hata hivyo, mahojiano hayo hayakuwahi kufanyika, na sasa kesi imefungwa rasmi.Kama ilivyoripotiwa awali, baba wa Nicki aliuawa Februari 2021 katika eneo la Long Island, New York alipokuwa akivuka barabara, baada ya kugongwa na gari lililoendeshwa na Polevich. Dereva huyo alikimbia eneo la tukio, lakini baadaye alikamatwa kwa kutumia CCTV Camera.
Polevich alikiri kosa la kuhusika na ajali hiyo pamoja na kukimbia eneo la tukio na kuharibu ushahidi, na alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela.

