Melinda French Gates amefichua sababu iliyomfanya kulazimika kuacha ndoa yake na
mume wake wa zamani bilionea, BillGates
Kwa mujibu wake, aliachana naye kwa sababu ndoa yao haïkuwa na uaminifu.
Alisema ukosefu wa uaminifu uliathiri, Melinda alifichua haya alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa mtangazaji wa kipindi cha The Late Show, Stephen Colbert.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 60 aliondoka katika ndoa yake ya miaka 27 na Bill, mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, mwaka wa 2021.
Hivi majuzi, Melinda amerudi kwenye ulingo wa umaarufu akitangaza kitabu chake kipya cha kumbukumbu, ambacho anaelezea kwa uwazi mabadiliko makubwa katika maisha yake, ikiwa ni pamoja na talaka yake maarufu Melinda na Bill wana watoto watatu pamoja.