Mwanaume aliyekuwa akitafutwa kwa zaidi ya miaka 20 kuhusiana na mauaji yaliyotokea mwaka 2004 nchini Marekani, Antonio Riaño, amekamatwa baada ya kubainika kuwa alikuwa akiishi Mexico na kufanya kazi kama askari polisi wa eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa za mamlaka, Riaño alihusishwa na mauaji ya kijana mwenye umri wa miaka 25 huko jimbo la Ohio, kabla ya kukimbia nchi hiyo na kurejea katika mji wake wa asili nchini Mexico. Akiwa huko, aliweza kuajiriwa kama polisi wa kawaida na kuishi maisha ya kawaida kwa muda mrefu bila kutambuliwa.
Kesi yake iliwahi kuorodheshwa kwenye orodha ya most wanted ya Butler County na hata kuangaziwa kwenye kipindi cha televisheni America’s Most Wanted. Hata hivyo, baada ya uchunguzi wa muda mrefu uliohusisha ushirikiano wa mamlaka za Marekani na Mexico, Riaño alikamatwa mwezi Agosti mwaka huu katika jimbo la Оахаса.
Kukamatwa kwake kumefunga safari ndefu ya zaidi ya miaka ishirini ya kukwepa haki, huku tukio hili likiibua maswali mazito kuhusu mifumo ya ukaguzi wa ajira katika vyombo vya usalama na uwezo wa wahalifu kubadilisha utambulisho wao kwenye nchi nyingine.

