Site icon Bongo Plus

Ally Hapi – Kazi za Rais samia hakuna mfano Afrika

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM *Ndugu. Ally Hapi (MNEC)amewataka wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Kuunga Mkono jitihada na kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa katika Wilaya ya Mkuranga, Hapi alifanya shughuli kadhaa ikiwa ni pamoja na kutembelea mashina ya wanachama wa CCM pamoja na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya stendi Mkuranga.

“Kwa mambo na kazi alizozifanya Rais wetu hakika anapaswa kuungwa mkono na kila mmoja wetu, kazi zake kwenye miradi ya maendeleo inaonekana na mama amegusa kila sekta, ukienda kwenye maji ametoa mabilioni ya fedha watu wapate maji, kwenye afya ndiyo usiseme kila kijiji na kila kata miradi ya vituo vya afya na zahanati zimejengwa kwaajili ya kuhudumia wananchi “alisema Hapi

Katika hatua nyingine Hapi amepongeza kazi inayofanywa na viongozi wa serikali ya wilaya ya Mkuranga katika kuwahudumia wananchi ikiwa ni kuunga mkono maono ya kiongozi mkuu wa nchi ambaye amedhamiria kuboresha maisha ya wananchi kwa vitendo.

Awali akieleza utekelezaji wa Ilani ya CCM, *Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mhe. Khadija Nasri Ally,* alisema licha ya halmashauri hiyo kuendelea kutenga fedha za maendeleo ya miradi mbalimbali lakini wameendelea kupokea fedha za miradi kutoka serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Exit mobile version