Site icon Bongo Plus

Angola Yajiondoa Upatanishi Mgogoro Wa DRC,M23

Angola imehitimisha jitihada zake za
upatanishi katika mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kati ya Jeshi la Serikali la FARDC dhidi ya kundi la M23.

Kundi la M23 linaloongozwa na Corneille Nangaa linaendelea na mapigano dhidi ya FARDC ambapo hadi sasa limefanïkiwa kuiteka miji mikuu ya mashariki mwa
DRC ikiwemo Goma, Bukavu, Nyabibwe, na Walikale.

Angola chini ya Rais wake, Joao Lourenço ilijitosa kuwa mpatanishi kati ya pande hizo, jitihada ambazo nazo zimegonga mwamba badala yake taifa hilo limetangaza
kujiondoa.

Katika taarifa iliyotolewa jana Machi 24, 2025 na lkulu ya Angola, imesema: “Angola inaona ni muhimu kujondoa katika jukumu la upatanishi wa mzozo huu ili kujikita zaidi
katika vipaumbele vya jumla vya Umoja wa Afrika (AU).”

Exit mobile version