Site icon Bongo Plus

Askari Feki Akamatwa Simiyu Akiwa na Sare ya Jeshi la Wananchi Zenye Cheo Cha Luteni

Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limemtia mbaroni mtu mmoja aitwaye Emmanuel Sulwa Mapana (24) akijulikana kwa jina maarufu (Mchambi) Mkazi wa Mtaa wa Sima, Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu akiwa na sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania zenye cheo cha luteni.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu imeeleza kuwa leo tarehe 14/02/2025 majira ya saa 6:30 mchana kikosi kazi cha kupambana na uhalifu na wahalifu Mkoa wa Simiyu kilifanikiwa kumkamata mtu huyo akiwa amevaa Kombati ya Jeshi la Wananchi Tanzania akiwa na gari aina ya Ractic yenye namba ya usajili T.560 DCS na mara baada ya kufanyiwa upekuzi alikutwa na Mkanda wa Jeshi la Wananchi na Laptop 01.

Aidha, Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa Emmanuel Sulwa Mapana alikuwa anatafutwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa kosa la kujifanya mtumishi wa serikali.

Exit mobile version