Wakati Simba ikitarajiwa kupaa jioni ya leo kuelekea Misri kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2024-2025, beki Lameck Lawi yupo zake Dar es Salaam na kikosi cha Coastal Union akijifua tayari kwa michuano ya Kagame huku mwenyewe akisema yeye ni mchezaji halali wa Coastal Union.
Lawi ambaye alikuwa wa kwanza kutambulishwa ndani ya Simba kwa mastaa wao wapya kuelekea msimu ujao, inaelezwa dili hilo limekufa kutokana na kukiukwa utaratibu wa usajili wake.
Akizungumza na Mwananchi, Lawi alisema ni kweli yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kambi kujiandaa na michuano ya Kagame inayotarajiwa kuanza kesho Jumanne.
“Ndio nipo Dar es Salaam na Coastal Union kwa sababu ni mchezaji wa hii timu, tumekuja hapa kwa ajili ya kambi tunajiandaa na michuano ya Kagame,” alisema Lawi.

