Site icon Bongo Plus

Biden Kumshawishi Trump Kuisaidia Ukraine.

Rais wa Marekani, Joe Biden anatarajia kumshawishi Rais mteule, Donald Trump kutoacha kutoa msaada kwa Ukraine atakapoingia madarakani, kwa mujibu wa mshauri wa usalama wa taifa wa Rais anayemaliza muda wake.

Trump ambaye mara kadhaa amekuwa akikosoa misaada ya Marekani kwa Ukraine, atazungumza na Biden siku ya Jumatano lkulu ya White House.

Marekani imetoa msaada wa dola bilioni 174 (TZS trilioni 465] kwa Ukraine kupambana na Urusi, huku Biden akishawishi washirika wengine wa NATO kuendelea kutoa msaada.

Exit mobile version