Site icon Bongo Plus

Bunge la Seneta lamjia juu Trump sakata la Venezuela

Bunge la Seneta nchini Marekani limewasilisha muswada wa kukomesha kufungwa kwa serikali ya Venezuela.

Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya vikosi vya Marekani kumkamata Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro katika shambulio la kijeshi tukio ambalo limepingwa na baadhi ya wabunge wa Seneta wakiituhumu serikali kwa kulipotosha Bunge juu ya sababu ya kukamatwa kwake.

Maseneta hao wameeleza kuwa lengo la muswada huo ni kupinga hatua za Trump juu ya matumizi ya nguvu za kivita zilizoanzishwa tangu utawala huo ulipoongeza shinikizo la kijeshi nchini humo, kwa mashambulizi dhidi ya boti karibu na pwani yake Septemba mwaka jana.

Muswada huo unalenga kumzuia Donald Trump kuchukua hatua zaidi za kijeshi dhidi ya Venezuela bila idhini ya bunge, huku wabunge wanaounga mkono wakisema kuwa hatua hiyo Italiheshimisha taifa hilo na kuwezesha matumizi ya sheria kushughulika na madai hayo.

Miongoni mwa Wabunge wanaounga mkono muswada huo, Rand Paul amesema kuwa kupitishwa kwa muswada huo ni hatua muhimu ya kusitisha matumizi makubwa ya mamlaka ya kivita dhidi ya mataifa mengine.

“Siwezi kukuhakikishia jinsi watakavyopiga kura, lakini hatua hii itaweka msingi wa matumizi ya njia bora katika kusimamia sheria ili kuimarisha ukaribu baina yetu na mataifa mengine,” amesema Paul.

Exit mobile version