Site icon Bongo Plus

Davido auza tiketi zote nchini Canada aweka historia tenah

Mkali wa Afrobeats kutoka Nigeria, @davido ameandika historia tena baada ya kuuza tiketi zote kwa ajili ya tamasha lake linalofanyika usiku wa leo katika ukumbi mkubwa wa Scotiabank Arena jijini Toronto, Canada. Tamasha hili ni sehemu ya muendelezo wa ziara yake ya kimataifa ya 5ive Alive Tour.

Scotiabank Arena ni moja ya kumbi maarufu zaidi nchini Canada, ikiwa na uwezo wa kubeba zaidi ya watu 19,000. Uuzwaji wa tiketi zote ni ishara ya wazi kuwa Davido anaendelea kujiimarisha kama mmoja wa wasanii hatari zaidi duniani kwa sasa, akiwa na ushawishi mkubwa wa kimuziki, mashabiki wengi, na uwezo wa kujaza kumbi kubwa nje ya bara la Afrika.

Huu ni ushahidi kuwa muziki wa Afrika umevuka mipaka na kwamba Davido ni sehemu ya wasanii wachache wanaoibeba bendera ya bara hili kwa mafanikio makubwa duniani.

 

Exit mobile version