Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mheshimiwa Innocent Shiyo na Wafanyakazi wa Ubalozi wa huo nchini Ethiopia mara baada ya kumaliza ziara yake nchini humo, tarehe 15 Februari, 2026.
Rais Dkt. Samia alikuwemo nchini humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne, ambapo pamoja na mambo mengine alishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika tarehe 14 na 15 Februari, 2026.
