Site icon Bongo Plus

Enock Aomba Msamaha na Mbosso Amjibu Kwaupendo

Kama sehemu ya mwitikio wa mahojiano ya jana ambayo Mbosso alikanusha madai ya kutokuwa karibu na Enock Bella Baad ya Yamoto Band, Enock Bella amechukua hatua ya kiungwana kwa kuandika ujumbe wa kuomba msamaha wa wazi kwenye Instagram.

Kwenye ujumbe wake, Enock aliandika:

“Kaka yangu @mbosso_kwanza nichukue nafasi hii kuomba RADHI hadharani kwa kukukwaza kwenye mahojiano niliyofanya mwaka jana… Naomba RADHI.”

Enock alisisitiza kuwa Yamoto Band haikuwa tu bendi ya muziki bali shule ya maisha, na akatoa wito kwa mashabiki wa muziki kuendelea kuwaunga mkono wasanii wao badala ya kuwagombanisha.

Kwa upande wake, Mbosso hakusita kujibu kwa mapenzi na ukaribu, akimkumbusha Enock jinsi alivyochangia kumrudisha kwenye muziki baada ya kuvunjika kwa Yamoto Band.

“Unajua kwa nini nipo hapa leo? Kwa sababu kauli yako moja ilinipa ujasiri… Love you so much bro

” aliandika Mbosso.

Tukio hili linaonyesha ukomavu wa wasanii wetu na mfano mzuri wa mshikamano unaoweza kurudishwa licha ya tofauti za awali. Room Number 3 si tu EP ya muziki, bali pia imekuwa chachu ya kuunganisha tena mioyo.

Exit mobile version