Site icon Bongo Plus

Feisal Salum Aongeza Mikataba Mpya na Azam FC hadi 2027

Kiungo nyota wa Klabu ya Azam FC, Feisal Salum ‘Feitoto’, amesaini rasmi mkataba mpya wa mwaka mmoja, na hivyo ataendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwaka 2027.

Feisal ambaye alikuwa anakaribia kumaliza mkataba wake wa awali (mwaka mmoja kubaki), amekuwa akihusishwa na vilabu mbalimbali, lakini sasa Azam FC imekata mzizi wa fitina kwa kumuweka ndani kwa muda mrefu zaidi.

Taarifa rasmi kutoka klabu hiyo imethibitisha kuwa nyota huyo ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Azam FC kinachojiandaa na msimu wa 2025/26 pamoja na mashindano ya kimataifa.

Exit mobile version