Tukio la kushangaza limeibua mjadala mkubwa nchini Nepal baada ya vijana wa kizazi cha Gen Z kurekodi na kusambaza video muda mfupi tu baada ya moto kuzuka kwenye jengo la bunge na makazi ya Waziri Mkuu KP Sharma Oli.
Video hizo, ambazo zimeenea haraka kwenye mitandao ya kijamii, zimekosolewa vikali na umma na wachambuzi, wakionyesha wasiwasi kuhusu mwenendo wa vijana na athari za utamaduni wa mitandao ya kijamii. Wengi wameeleza kuwa kitendo hicho ni cha kutojali na ni ukosefu wa heshima katika wakati ambapo nchi inakumbwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa na maandamano ya vurugu yaliyopelekea vifo vya raia 19.
Mamlaka za usalama zimethibitisha kuwa zinachunguza tukio hilo, huku wananchi wakibaki wameduwaa na ujasiri wa vijana hao waliogeuza machafuko kuwa maudhui ya mitandao.

