
Kwenye posti yake ya leo kwenye
instagram, Haji Manara amezua gumzo baada ya kushea video ya CCTV inayomuonyesha mtu akimshambulia
mwenzake kwa kipigo na kutumia silaha ya bunduki.
Manara alielezea kusikitishwa kwake na hali hiyo, akihoji iwapo kweli bado kuna watu wanafikia hatua ya kugombania wanawake kwa kutumia silaha.
“Nchi hii bado kuna viumbe wanagombea wanawake hadi kutoleana silaha? Wanawake hawa hawa au wale wa peponi tunaowasoma kwenye vitabu vitukufu?” aliandika @HajisManara, akiashiria kuwa kuna matumizi mabaya na yasiyo na maana ya silaha kwa baadhi ya watu.
Alisisitiza kuwa matukio kama haya ni ishara
“ulimwengu wa kishamba” na matumizi ya ovyo ya bunduki kwa sababu zisizo na msingi. Manara alihitimisha ujumbe wake kwa kukosoa tabia hiyo, akisema ni
“ulimwengu wa kishamba” na ni upotofu wa imaadili.

