Site icon Bongo Plus

Hakuna Uthibitisho wa Mwanamke Aliyekuja Kutoka Nchi Isiyo Kuepo.

Video inayosambaa mtandaoni ikimuonyesha mwanamke akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa JFK nchini Marekani akiwa na pasipoti kutoka “Torenza” imebainika kuwa habari ya uongo. Uchunguzi wa vyombo vya habari kama NDTV na industan Times umeonyesha kuwa nchi ya “Torenza” haipo duniani, na video hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Artificial Intelligence (Al).

Wataalamu wanasema video hiyo ni mfano wa kile

kinachoitwa Al Hoax – maudhui ya uongo yanayotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ili kuonekana kama ya kweli. Inadaiwa kuwa simulizi hii inafanana na hadithi ya zamani ya “The Man from Taured,” ambayo nayo ilikuwa ya kubuni.

Wataalamu wa habari wanashauri watumiaji wa mitandao kuwa waangalifu, kuthibitisha chanzo cha video au taarifa kabla ya kuamini au kusambaza.

Hakuna mwanamke kutoka “Torenza” aliyepatikana Marekani. Video hii ni ya kubuni, ishara kuwa teknolojia ya Al inaweza kudanganya macho na akili zetu kama hatutakuwa makini.

Exit mobile version