Taarifa mpya zinaonyesha kuwa Iran bado inaendelea kusafirisha mafuta licha ya vizuizi vya kijeshi vya Marekani kwenye eneo la mlango Bahari wa Hormuz.
Kwa mujibu wa data za kampuni ya ufuatiliaji wa meli Tanker Trackers, Iran imefanikiwa kupakia takribani mapipa milioni 4.6 ya mafuta ghafi kwenye bandari zake za usafirishaji. Aidha, ripoti zinaonyesha kuwa mapipa mengine karibu milioni 4 yamefanikiwa kupenya na kupita vizuizi vya Marekani.
Wataalamu wanasema Iran imekuwa ikitumia mbinu za hali ya juu kukwepa vizuizi, ikiwemo:
1. Kuzima mifumo ya utambuzi wa meli (“going dark”). 2. Kubadilisha bendera na umiliki wa meli. 3. Kutumia mitandao ya siri ya usafirishaji wa mafuta.
Ripoti nyingine kutoka vyanzo vikubwa vya Habari duniani kama Aljazeera zinaonyesha kuwa tangu kuanza kwa kizuizi, yaani blockade, mamilioni ya mapipa ya mafuta tayari yamevuka na kuingia sokoni, jambo linaloonyesha kuwa utekelezaji wa vizuizi hivyo una changamoto.

