Mke wa staa wa Bongo Fleva Juma Jux, Priscilla, ameweka wazi furaha yake kubwa kwa mara ya kwanza baada ya kujifungua mtoto wao wa kwanza, Rakeem Mkambala, nchini Canada.
Kupitia instagram, Priscilla ameshare baadhi ya video akiwa hospitalini muda mfupi baada ya kujifungua. Katika video hizo, mama wa Priscilla ameonekana akiwa na tabasamu la furaha na hisia zisizofichika, ishara ya safari mpya ya maisha yake kama bibi.
Mashabiki wamefurahia kuona upande huo wa kifamilia wa Priscilla na Jux, huku wengi wakimiminika kwenye comment kuwatakia heri njema na baraka tele kwa mtoto wao mchanga.
Kwa sasa, Jux na Priscilla wameingia rasmi katika ukurasa mpya wa maisha yao, na mtoto wao Rakeem Mkambala tayari ameongeza sababu nyingine ya upendo katika familia yao.

