
Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Dr Wilbroad Slaa anashikiliwa na jeshi la polisi nchini humo akikabiliwa na makosa ya uhaini.
Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache tangu, Mkuu wa Jeshi la polisi, IGP Camilius Wambura, kutamka kuwa kuna watanzania wenye nia ya kumpindua Rais Samia Suluhu Hassan.

