Site icon Bongo Plus

KATAMBI KUFUNGA MAFUNZO YA ASKARI 1000 ZIMAMOTO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Patrobas Katambi amewasili wilayani Handeni Mkoani Tanga ambapo anatarajiwa kufunga Mafunzo ya Awali,Kozi Na.6/2026 katika Chuo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambapo askari 1000 wanahitimu mafunzo hayo leo,tarehe 24/6/2026.

Mafunzo hayo yanayohitimishwa leo yanajumuisha Wataalamu katika kada za Uzimaji Moto wa Kemikali,Maokozi ya Angani,nchi kavu na majini ambapo wanaume wapo 651 na wanawake 349.

Exit mobile version