Site icon Bongo Plus

Korea Kaskazini Yazidi Ukandamizaji wa Haki za Binaadamu.

KoreaKaskazini: Korea Kaskazini inaelezwa kuzidisha ukandamizaji wake wa haki za binadamu na raia wa taifa hilo wanazidi kukata tamaa na kuna pia ripoti za watu wanakufa kwa
njaa katika baadhi ya maeneo ya nchi, huku hali ya uchumi ikizidi kuwa mbaya.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa ofisi ya Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk katika mkutano wa kwanza wa haki za
binaadamu kuhusu Korea Kaskazini tangu mwaka 2017.

Kiongozi huyo wa ofisi ya Umoja wa Mataifa amesema taarifa walizonazo ni kwamba watu wamekuwa na hofu ya kufuatiliwa na serikali, kukamatwa,kuhojiwa na kuwekwa kizuizini.

 

Exit mobile version