Site icon Bongo Plus

Kuna nafasi kubwa ya Yanga SC kucheza robo fainali ya ligi ya mabingwa endapo tutashinda mchezo ujao dhidi ya CR Belouzidad,

Kuna nafasi kubwa ya Yanga SC kucheza robo fainali ya ligi ya mabingwa endapo tutashinda mchezo ujao dhidi ya CR Belouzidad, hakuna namna nyingine ya kufanya hivyo ni lazima mchezo huo tutapate alama tatu hizo, kwenye kundi letu kila timu inaonesha kuwa ina uwezo wa kufuzu kwa lugha rahisi kila mtu ni mbabe” alikamwe Meneja Habari na Mawasiliano Young Africans SC

Licha ya kuwa na ratiba ngumu, tutahitaji kucheza mechi nyingine zilizopo mbele yetu ili kujenga utimamu wa mwili wachezaji wetu kuelekea mchezo huo. hivyo hakuna sababu ya kudeka deka, mchezo wetu na Polisi Tanzania FC ipo pale pale Chamazi. Kule Morogoro tumewaonjesha kidogo sumu ambayo tumeandaa kwa ajili ya mwarabu.” alikamwe Meneja Habari na Mawasiliano Young Africans SC

“Tulianza na mtoko wa Max, Aziz Ki, Bacca na GSM, Mchezo wetu wa awali na CR Belouizidad wengi tulifurahishwa na namna ambavyo timu ilicheza lakini tukahuzunishwa na matokeo. Mchezo huu tunakwenda na agenda kadhaa, kushinda na kulipa deni la magoli matatu.

“Uongozi na benchi la ufundi tumekubaliana kama taasisi Jumamosi ikawe Pacome Day, ukisema Pacome Day mwisho unamalizia Kitaalamu zaidi, unaweza kupaka rangi kichwani au kwenye ndevu. Kama huwezi kupaka rangi basi unaweza kujichora chochote na wanawake wanaweza kupaka kucha rangi.” alikamwe Meneja Habari na Mawasiliano Young Africans SC

 

“Kilichosaidia CR Belouizdad ni wingi wa mashabiki wao, ukweli ni kwamba sisi sio wanyonge kimsingi hatuwezi kufanikiwa bila uwepo wa mashabiki wetu ambao kwa dakika zote tuwe na sapoti kubwa, kuanzia dakika ya kwanza mpaka dakika ya mwisho, tusishangilie matokeo tunapaswa kushangilia kila dakika kuhakikisha mwarabu anapagawa”

“Jumamosi sio mchezo wa kitoto, ni mechi ya kikubwa kweli. Benchi la ufundi kimsingi limejiandaa vya kutosha kwa upande wa mashabiki tunapaswa kufika na hasira ya kweli kila anayeamini analo jambo ambalo linaweza kusaidia timu yako kushinda basi lifanye,ruksa popote ulipo usimuogope mtu wewe fanya. Hakuna masihara mchezo ujao, tukitoka sare basi ujue tumeisha”alikamwe Meneja Habari na Mawasiliano Young Africans SC

Exit mobile version