Site icon Bongo Plus

Madereva Bodaboda 759 Wafariki Dunia Kwa Ajali Ndani Ya Miaka 3

Jumla ya madereva bodaboda 759 wamefariki dunia kutokana na ajali kati ya mwaka 2022 na 2024.

Hayo yamesemwa leo, Jumanne Februari 11, 2025, bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Fatuma Hassan Toufig.

Mbunge huyo aliuliza ni wananchi wangapi wamepoteza maisha kutokana na ajali za pikipiki kati ya mwaka 2022 na 2024.

Mbali na vifo vya madereva hao, Sillo amesema kuwa wananchi wa kawaida 283 pia wamefariki dunia kutokana na ajali za bodaboda katika kipindi hicho.

Exit mobile version