NI KWELI MAFAHARI WAWILI HAWAISHI ZIZI MOJA?
Huko mtaani wanasema mafahari wawili hawaishi zizi moja? Huku kwetu mbugani, mafahari wawili wanaweza kuishi zizi moja tena bila shida na mambo yakawa sawa. Je? hawa mafahari wanaweza kuishi zizi moja kwa namna gani?
1. WANAISHI KWENYE KUNDI LINALOITWA PRIDE.
Simba wanaweza kuishi kwenye kundi ambalo kitaalamu linajulikana kama PRIDE. Hili kundi linaweza kuwa na madume mpaka watatu, wakiwa na majike na watoto wao. Kundi hili linaweza kufika mpaka idadi ya simba 40 au zaidi kutegemeana na mazingira husika.
2. WANAISHI PIA KWENYE KUNDI LINALOJULIKANA KAMA COALITION.
Simba wanaweza kuishi kwenye kundi ambalo kitaalamu hujulikana kama LION COALITION ama wengine huamua kuwaita COALITION BROTHER’S.
Hawa huwa ni simba wenye ukaribu kwa maana ya vinasaba ama wanaweza wasiwe na vinasabab vya karibu na wakaamua kuishi pamoja. Hili kundi linaweza kuwa na simba dume mpaka 7 wakimiliki jike au majike. Majike au jike kwenye kundi hili, hulazimika kulala na kila dume.
KWANINI SIMBA JIKE ANAKUBALI KUJAMIIANA NA KILA DUME KWENYE KUNDI?
Simba dume huwa halei watoto ambao sio wake, kwa maana hiyo, simba jike atalazimika kufanya hivyo kwa lengo la kulinda watoto wake watakaozaliwa wasiuawe. Watoto watakaozaliwa kwenye hilo kundi watakuwa ni mali ya madume wote na sio dume mmoja.
KUNDI HUWA NA KIONGOZI ANAYELISIMAMIA.
Kundi hili (Coalition) huwa na kiongozi wao ambaye ni dume aliyeunganisha wengine. Huyu ndo huwa kiongozi wao ambapo husimamia kila kitu kwenye kundi na kuongoza wenzie.
Hata wanapoanza kumpanda jike akishakuwa kwenye joto, basi huyu kiongozi ndo hutangulia kufungua dimba, kisha wengine hufuata. Hapa ndo kuna lile suala la DORMINANCE. Itifaki lazima izingatiwe