Site icon Bongo Plus

Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche Akamatwa na Jeshi la Polisi.

I’mInadaiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara John Heche amekamatwa muda mfupi uliopita leo, Jumatano Oktoba 22.2025 akiwa anaingia kwenye viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam

Akizungumza na Wanahabari kuhusiana na hilo, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amedai kuwa Heche amekamatwa ghafla alipokuwa anaingia Mahakamani hapo lakini hadi sasa uongozi wa chama hicho haujui sababu ya kukamatwa kwake,

Amesema amepokea simu kutoka kwa mmoja wa wasaidizi wa Makamu Mwenyekiti huyo na kumueleza kuwa Heche amepelekwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati (Central Police) Dar es Salaam, na kwamba kwa sasa Mawakili wanaelekea kituoni hapo kufuatilia sababu za kukamatwa kwake.

Exit mobile version