Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia CCM.
Fomu hiyo ameichukua leo Juni 28, 2025 katika Ofisi za CCM Wilaya ya Arusha Mjini na kukabidhiwa na Katibu wa CCM wa wilaya hiyo.

