Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameagiza Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kuhakikisha ofisi ya Rais wa shirikisho hilo inakabidhiwa kwa Hasheem Thabeet ndani ya siku mbili kabla ya Jumatatu. Agizo hilo amelitoa Machi 13, 2026 wakati akifunga mkutano wa Baraza la Michezo la Taifa na viongozi wa vyama vya michezo uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
