Mwanamke mwenye umri wa miaka 40 na kuendelea yupo katika hatari ya kupata matatizo mbalimbali ya kiafya.
Matatizo hayo ni pamoja na saratani kama vile ya shingo ya uzazi na matiti na magonjwa yasiyoambukiza kama magonjwa ya moyo, kisukari, kiharusi, magonjwa sugu ya figo, unene uliokithiri na magonjwa ya akili.
Pia magonjwa ya kuambukiza, ikiwamo maambuzi ya virusi vya Ukimwi (VVU), TB, malaria na magonjwa yanayoshambulia viungo vya uzazi,
ikiwamo yanayoenea kwa njia ya kujamiiana.
Kuna mambo 10 ambayo wanawake wazee paswa kushikamana nayo ili kujikinga na magonjwa na hatimaye kuwa timamu kiafya na kuishi maisha marefu.
Moja, inahitajika kuepuka ulaji holela wa vyakula, ikiwamo chumvi na sukari nyingi, wanga na mafuta mengi na badala yake wale zaidi mbogamboga na
matunda.
Umri unaposonga na kinga nayo hushuka, hivyoni rahisi kupata magonjwa yanayoshambulia mfumo
wa chakula, ikiwamo usugu wa vimelea katika vyakula. Kunywa maji ya kutosha angalau glasi 10 kwa siku.
Fanya mazoezi mepesi na kazi
zinazoushughulisha mwili. Kwa siku angalau fanya mazoezi ya kutembea dakika 30 hadi 60 au tembea kilomita mbili katika siku tano za wiki. Fanya
shughuli za nyumbani kama za bustani na usafi wa mazingira ya ndani.
Fanya uchunguzi wa kiafya, muhimu kujitokeza wakati wa uchunguzi wa matatizo ya kiafya yanayomgusa mwanamke moja kwa moja, ikiwamo
saratani ya mlango wa uzazi namatiti
Pia fanyau chunguzi wa jumla angalau mara moja kwa miezi sita zingatia elimu ya afya, hasa zile za kampeni za kitaifa, ikiwamo namna ya kujichunguza matiti na maeneo ya uzazi. Lengo ni kuweza kubaini ishara za awali za saratani, ikiwamo ya matiti na shingo ya uzazi.