Mashtaka 120 Mapya Yaibuliwa Dhidi ya P Diddy

Mashtaka 120 Mapya Yaibuliwa Dhidi ya P diddy.

Sean Combs, maarufu kama P Diddy au
Puff Daddy, anakabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono kutoka kwa watu 120 wapya, wakiwemo wanaume 60 na wanawake 60.

Mawakili wanaowakilisha waathiriwa wanasema baadhi ya waathiriwa walikuwa
watoto wakati wa matukio hayo, huku mmoja akidai kuwa alinyanyaswa akiwa na umri wa miaka tisa.

Tuhuma hizi zinaanzia mwaka 1991 hadi mwaka huu. Tony Buzbee, wakili wa waathiriwa, alisema anatarajia kesi hizo kufunguliwa ndani ya mwezi mmoja ujao, na
kwamba sehemu kubwa ya mashtaka haya yatapelekwa mahakamani kwenye majimbo ya New York na Los Angeles.

Diddy tayari anakabiliwa na mashtaka mengine ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya biashara ya ngono, ambapo alikana mashtaka hayo na kusema madai hayoni
ya uwongo na skendo za kumchagua. Wakili wakebwamesema baba huyo wa watoto saba tathibitisha kutokuwa na hatia mahakamani.

P Diddy amekuwa kizuizini tangu Septemba 17, 2024, baada ya kukana mashtaka ya kulazimisha wanawake kushiriki matukio ya kingono wakiwa wamelewa, pamoja
na mashtaka mengine ya ulanguzi wa wanawake wanaojiuza na njama za ulaghai.

Mawakili wake wameomba dhamana ya dola milioni 50 ili awekwe chini ya ulinzi wa kifaa cha GPS akiwa nyumbani kwake Florida,
lakini onmbi hilo limekataliwa hadi sasa.

Sean Combs alianzisha lebo ya Bad Boy Records mwaka 1993 na ni mmoja wa mabosi wakubwa kwenye tasnia ya
muziki wa hip-hop, akiwa ameshinda tuzo tatu za Grammy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button