Site icon Bongo Plus

Mazungumzo yakusitisha mapigano DR Congo yahamishiwa Uswisi, kuanza leo

Duru mpya ya mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mapigano yanayoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inaanza leo nchini Uswisi, huku wapatanishi kutoka Marekani na Qatar wakitarajiwa kushiriki.

Mazungumzo hayo yanawakutanisha wawakilishi wa serikali ya DRC na waasi wa kundi la M23, ambao wanadaiwa kuungwa mkono na Rwanda, ingawa rais wa nchi hiyo Paul Kagame amekanusha hilo mara kadhaa, yakilenga kufikia muafaka wa kudumu wa kusitisha mapigano.

Taarifa zinaeleza kuwa mazungumzo hayo yamehamishiwa Uswisi kutoka Qatar, ambako yalikuwa yakiendelea tangu Aprili 2025, kufuatia changamoto za kiusalama zinazoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati.

Akizungumza na gazeti la The New Times, msemaji wa M23, Oscar Balinda amesema duru hiyo mpya itajikita zaidi katika kuhakikisha misaada ya kibinadamu inawafikia wananchi wanaoishi katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo.

“Lengo kubwa kwa sasa ni kuona wananchi wanapata msaada wa haraka wa kibinadamu, hii ni sehemu ya itifaki ya tatu kati ya nane zilizokubaliwa wakati wa mazungumzo ya Doha,” amesema Balinda.

Exit mobile version