Mwenyekiti mstaafu wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akisalimiana na kumpa pole Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba leo Jumanne Machi 25, 2025 kwa kufiwa na mkwe wake katika Kanisa la KKKT Usharika wa Boko jijini Dar es Salaam.
Hii ni kwa mara ya kwanza Mbowe kuonekana katika shughuli ya kijamii tangu atoke katika wadhifa wa mwenyekiti Januari 22, 2025.