Site icon Bongo Plus

Mbunge-Dodoma MjiniJana nimekabidhi Gari la kubeba wagonjwa (𝘼𝙢𝙗𝙪𝙡𝙖𝙣𝙘𝙚) lenye thamani ya Tsh 120,000,000 kwa ajili ya Hospital ya Wilaya ya Dodoma iliyopo kata ya Nala.

Tunamshukuru Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa Fedha kiasi Cha Shilingi Bilioni 1.9 za ujenzi wa Hospital hii ya kihistoria.Dodoma haikuwahi kuwa na Hospital ya Wilaya hapo awali kwa kuwa huduma nyingi zilikuwa zinatolewa kupitia Hospital ya Rufaa ya Mkoa(𝙂𝙚𝙣𝙚𝙧𝙖𝙡 𝙃𝙤𝙨𝙥𝙞𝙩𝙖𝙡).

Nawashukuru pia Kampuni ya GF Trucks Kwa gari hili la kisasa la kubebea wagonjwa lenye vifaa vya kisasa;

1. Kiti mwendo
2. ⁠Sanduku la huduma ya kwanza
3. ⁠Sehemu ya kunawa Mikono na Kuosha
4. ⁠Siti ya nyuma ya mtoa huduma
5. ⁠kitanda cha kubebea wagonjwa
6. ⁠Mashine ya kupima mapigo ya moyo
7. ⁠Vifaa vya kupima Mapigo ya moyo
8. ⁠Switch ya Umeme
9. ⁠kifaa cha kuangalia koo
10. ⁠Kifaa cha kusaidia kupumua
11. ⁠Tubu ya hewa kwa ajili ya kupumua
12. ⁠mashine ya ufuatiliaji wa shinikizo la damu
13. ⁠kifaa cha ku support shingo
14. ⁠kifaa cha kuanzisha mapigo ya moyo yaliosimama
15. ⁠tray ya dawa ya Chuma
16. ⁠kifaa cha kukandamizia ulimi
17. ⁠Mpira wa kunyonya (suction)
18. ⁠kifaa cha kusikia kifua na mapigo ya moyo
19. ⁠mashine kwa ajili ya dawa zinazotolewa kwa njia ya hewa
20. ⁠mashine ndogo ya kutakasa vifaa
21. ⁠Taa

Exit mobile version