Site icon Bongo Plus

Mbunge Wa Moshi Mjini Anusurika na Kifo

Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya CCM, Ibrahim Shayo (Ibra Line), amepata ajali ya gari katika eneo la Kirinjiko, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro wakati akiwa katika ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt Mwigulu Lameck Nchemba.

Ajali hiyo imetokea leo February 18, 2026 ambapo Mbunge huyo amenusurika kifo akiwa na Dereva wake pamoja na Katibu wake, Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa, amesema taarifa za awali ni kwamba gari hilo lilipasuka tairi la mbele na kupoteza mwelekeo.

Exit mobile version