Site icon Bongo Plus

Mchezaji Trejo Apoteza Mke na Watoto Wawili Tetemeko Venezuela

Taarifa za kusikitisha na majonzi makubwa yaliyomkuta mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina anayekipiga katika klabu ya Club Sport Marítimo La Guaira, Lucas Trejo aliyepoteza familia yake mke Yanina pamoja na watoto wake wawili Aarona na Ainhoa katika tetemo kubwa la ardhi liiloikumba Venezuela wiki iliyopita na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.

Trejo alikuwa kambini na timu yake jijini Caracas wakati matetemeko hayo mawili yalipotokea, alirejea haraka nyumbani kwake mjini La Guaira na kushiriki kwa siku kadhaa katika juhudi za kutafuta familia yake chini ya vifusi, huku akisaidiwa na marafiki na wachezaji wenzake.

Baada ya siku kadhaa za matumaini, klabu yake ilithibitisha kupitia ujumbe wa mitandao ya kijamii kuwa mke na watoto wake wote wamefariki dunia. Tetemeko hilo, ambalo limeua zaidi ya watu 1,400 nchini Venezuela.

Exit mobile version