Site icon Bongo Plus

MH JUMA AWESO AMEFANYA KIKAO NA WATUMISHI WA CHUO CHA MAJI

Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Aweso, amefanya kikao kazi na watumishi wa Chuo cha Maji pamoja na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu ambayo mchakato aliuanzisha na Rais Samia kuridhia kutoa fedha na tayari Ukarabati wa Mabweni umekamilika na sasa kazi ya ujenzi wa Maktaba kubwa ya kisasa unaendelea.

Waziri Aweso ameridhishwa na hatua ujenzi ulipofika na kuipongeza menejimenti ya Chuo cha Maji kwa kutekeleza maelekezo yake kwa vitendo na zaidi akimshukuru Mhe Rais Samia kwa kuridhia na kutoa fedha za Ukarabati wa Chuo hiki.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Cyprian Luhemeja, ameeleza kuwa yeye ni mdau mkubwa wa Chuo cha Maji. Amezungumzia jinsi alivyokuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) na kuajiri wafanyakazi zaidi ya 1200 kutoka Chuo cha Maji.

Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt Adam Karia amemshukuru Waziri wa Maji kwa kutoa mchango mkubwa katika kukiendeleza Chuo, tangu akiwa Naibu Waziri wa Maji mpaka sasa. Aliendelea kumshukuru waziri kwa kumwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasan Shilingi Bilioni 1.5 za kukarabati mabweni yaliokuwa yamechakaa.

Exit mobile version