Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. @jmkikwete ambaye pia ni Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika (AU) kwa Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu akifurahia jambo na Mhe. @KagutaMuseveni, Rais wa Uganda mara baada ya mkutano wao uliofanyika Ikulu ya Nakasero, Aprili 07, 2026.
Wengine pichani ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli na Balozi wa Jamhuri ya Uganda hapa nchini Mhe. Kanali (Mst.) Fred Mwesigye.
Mkutano wa viongozi hao wawili ulijikita katika kujadili hali ilivyo nchini Sudan Kusini ambapo msisitizo juu ya umuhimu wa mazungumzo kati ya pande husika ulitolewa.
Mara baada ya mkutano huo, Rais Kikwete aliendelea na ziara yake rasmi kwenda Juba, nchini Sudan Kusini kupitia Nairobi, kama sehemu ya ziara yake ya kikanda
