Rais wa Marekani, Donald Trump, ameionya Israel kuendelea kurusha makombora kwa Taifa la Iran akisema kufanya hivyo ni ukiukwaji mkubwa:
Tump kupitia mtandao wake wa Truth ameandika:-
“Israeli, msitupe mabomu hayo. Mkifanya hivyo ni ukiukaji mkubwa. Warudisheni marubani wenu nyumbani sasa hivi.”
Kauli hiyo imeibua hisia kali duniani, huku viongozi wa kimataifa wakitaka pande husika kuchukua tahadhari kubwa na kuepuka hatua zozote zitakazosababisha maafa kwa raia wasio na hatia
