Mtoto aliyefahamika kwa jina la Oscar James (9) aliyekuwa Mwanafunzi wa Darasa la Nne na Mkazi wa Mtaa wa Tangi la Maji, Kata ya Kingolwira, Manispaa ya Morogoro amefariki baada ya kudaiwa kujinyonga nyumbani kwao. Baba Mdogo wa Marehemu, Masaga Sagana amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 2, 2026 majira ya saa mbili usiku wakati Mama wa Mtoto huyo akiwa kazini ambapo amesema Mtoto huyo alikuwa nyumbani pamoja na Wadogo zake wawili.
Mwenyekiti wa Mtaa huo, Mohamed Abdalah amesema kabla ya tukio Mtoto huyo alikuwa akitafuta fedha kwa ajili ya mahitaji ya Shule, huku akitoa wito kwa WNazazi na Walezi kutenga muda wa kuzungumza na Watoto wao ili kufahamu changamoto wanazopitia. Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi wa awali unahusisha kutopatiwa kwa wakati kalamu aliyokuwa akihitaji kwa maandalizi ya mtihani wa Darasa la Nne.

