Site icon Bongo Plus

Mwanamuziki kutoka Nigeria, @patorankingfire, leo ameitembelea klabu maarufu ya soka Borussia Dortmund kwenye kambi yao ya mazoezi iliyopo Fort Lauderdale, Florida, Marekani.

Mwanamuziki kutoka Nigeria, @patorankingfire, leo ameitembelea klabu maarufu ya soka Borussia Dortmund kwenye kambi yao ya mazoezi iliyopo Fort Lauderdale, Florida, Marekani. Kwa sasa klabu hiyo inashiriki michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu (FIFA Club World Cup), ikiwakilisha bara la Ulaya.

Kupitia kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii, Borussia Dortmund wamechapisha picha mbalimbali zikimuonesha Patoranking akisalimiana na wachezaji wa timu hiyo na kubadilishana nao mawazo. Klabu hiyo imetoa taarifa ikieleza kufurahishwa na uwepo wa msanii huyo uwanjani leo, wakieleza kuwa ilikuwa heshima kubwa kumkaribisha.

Licha ya mafanikio yake katika muziki wa Afrobeats, Patoranking pia ni mdau mkubwa wa michezo nchini Nigeria. Ameshiriki kwa vitendo kuinua vipaji vya vijana kwa kujenga uwanja wa mpira wa miguu, ikiwa ni juhudi za kuunga mkono maendeleo ya michezo na kuwapa vijana fursa ya kukuza vipaji vyao

 

Mwanamuziki kutoka Nigeria, @patorankingfire, leo ameitembelea klabu maarufu ya soka Borussia Dortmund kwenye kambi yao ya mazoezi iliyopo Fort Lauderdale, Florida, Marekani.

Exit mobile version