Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb), ameshuhudia utiaji saini wa makubalino ya ufadhili wa dola za Marekani milioni 225 kati ya @crdbbankplc na Benki ya @mufgbk_official ya Japan, kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa miradi yenye mlengo wa kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi. Benki ya CRDB imewakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Abdulmajid Nsekela na kwa upande wa MUFG Bank, mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji anayesimamia Masoko, Bw. Christopher Marks.
Tukio hilo limefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington D.C nchini Marekani, Kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ambapo Mhe. Dkt. Nchemba anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mikutano hiyo na kushuhudiwa pia na Waziri wa Nchi, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na Benki ya CRDB

