Sean “Diddy” Combs anadaiwa kutoroka
kwa siri Los Angeles baada ya mauaji ya rapa Notorious B.I.G. Machi 9, 1997, kwa msaada wa maafisa wa LAPD, kulingana na madai mapya ya Kirk Burrowes, mwanzilishi
mwenza wa Bad Boy Entertainment.
Kwenye kesi aliyofungua, Burrowes anadai kuwa Diddy, akiwa amepaniki lakini salama, aliharakisha kuondoka badala ya kuwafariji familia ya Wallace au wafanyakazi wa
Bad Boy. Burrowes anasema Diddy alimtafuta.mfanyabiashara mashuhuri Clarence Avant, ambaye kwa ushawishi wake alivwezesha kutoroshwa kwa Diddy kupitia
gari la polisi hadi uwanja wa ndege binafsi.
Kesi hiyo pia inamshutumu Diddy kwa maombolezo ya kinafiki baada ya kifo cha Wallace, ikidai kuwa kwa siri, yeye na wakili wake walimshinikİza Burrowes awape
mkataba wa mwisho wa Notorious B.l.G., ambao ulikuwa unampa udhibiti zaidi wa kifedha.
Diddy bado hajajibu rasmi madai haya mazito, lakini kesi hiyo imeongeza shinikizo kubwa dhidi yake katika kipindi hiki ambacho anakabiliwa na tuhuma mbalimbali za
unyanyasaji na vitisho.